Messi na Ronaldo hawafui dafu Kwa Mayweather

Wachezaji wa soka hata hivyo wametawala orodha ya wachezaji 10 tajiri zaidi duniani

Messi na Ronaldo hawafui dafu Kwa Mayweather

Wachezaji wa soka hata hivyo wametawala orodha ya wachezaji 10 tajiri zaidi duniani

06 June 2018 Wednesday 16:45
Messi na Ronaldo hawafui dafu Kwa Mayweather

Floyd Mayweather ametetea kiti chake baada ya kuongoza tena katika orodha ya wanamichezo wenye mkwanja mrefu zaidi duniani.

Mkwanja mrefu alioingiza Mayweather kutoka kwenye pambano na Conor McGregor umemfanya kuongoza orodha hii kwa mara ya nne ndani ya miaka 7, ameongoza na $ 285M, huku $275m zikitokana na kazi yake huku $ 10M zikitokana na dili.

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amedondoka nyuma ya mpinzani wake Lionel Messi, Ronaldo ameingiza $ 108 M wakati Messi akiwa ameingiza $ 111M wakifuatiwa na Conor McGregory na Neymar.

LeBron James (basketball), Roger Federer (tennis), Stephen Curry (basketball), Matt Ryan (American football) na Matthew Stafford (American football) wamefunga Top 10.

Pia kwa mara ya kwanza tangu 2010 hakuna mwanamichezo wa kike aliyeingia kwenye orodha hii.

Mara nyingi Serena Williams huwa anaingia lakini mwaka jana alijifungua mtoto hivyo alikaa kando ya mchezo wa Tennis ambao huwa unamwingizia mkwanja mrefu

Hii ndio Top 10

1. Floyd Mayweather - ngumi ($285m)

2. Lionel Messi – mpira wa miguu ($111m)

3. Cristiano Ronaldo - mpira wa miguu ($108m)

4. Conor McGregor - ngumi ($99m)

5. Neymar - mpira wa miguu ($90m)

6. LeBron James - kikapu ($85,5m)

7. Roger Federer - tennis ($77.2m)

8. Stephen Curry - kikapu ($76.9m)

9. Matt Ryan - American football ($67.3m)

10. Matthew Stafford - American football ($59.5m)

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.