Michael Wambura aachiwa, kurejesha fedha

Michael Wambura aachiwa, kurejesha fedha

08 October 2019 Tuesday 05:40
Michael Wambura aachiwa, kurejesha fedha

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA makamu wa rais wa shirikisho la soka nchini (TFF), Michael Wambura ameachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu baada ya kuingia makubaliano na Jamhuri ya kulipa zaidi ya milioni 100 ambazo alijipatia isivyo halali.

Uamuzi huo ulitolewa Oktoba 7, 2019 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina.

Wambura atalipa fedha hizo kwa awamu tano tayari Oktoba 7, 2019 amelipa milioni 20.

Februari 11, 2019 Wambura alifikishwa mahakamani hapo, akikabiliwa na mashtaka 17 likiwemo la kutakatisha fedha zaidi ya milioni 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.