Michael Wambura ajisalimisha kwa DPP akiri makosa

Michael Wambura ajisalimisha kwa DPP akiri makosa

02 October 2019 Wednesday 14:50
Michael Wambura ajisalimisha kwa DPP akiri makosa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yake

Wambura alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Februari 11, mwaka huu, akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya milioni 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.

Leo Oktoba 2, 2019 Wambura amedai hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa aliandika barua kwa DPP ili kuomba msamaha na kukiri makosa yake hivyo aliuomba upande wa mashtaka kufuatilia ili aweze kupata haki yake.

"Niliandika barua kwa DPP ili kuomba msamaha na kukiri makosa yangu hivyo ninasubiri majibu,"amesema Wambura.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amesema analifanyia kazi kwa haraka zaidi suala hilo.

Baada ya maelezo hayo Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Katika shtaka la kwanza ambalo ni la kughushi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 6, 2004, sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Siku hiyo hiyo, Wambura kwa nia ya kutapeli alitengeneza barua ya kughushi ambayo haina kumbu kumbu namba akionyesha imeandikwa na E Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.

Katika shtaka la kutoa na kuwasilisha nyaraka ya uongo, mshtakiwa alitoa barua iliyokuwa haina kumbu kumbu namba ya Julai 6, 2004, akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na E. Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck System Ltd, akionyesha kuwa anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, kuanzia shtaka la tatu hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi cha zaidi milioni 95, kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na riba kutoka kwa kampuni ya Jeck System Ltd huku akijua kuwa siyo kweli.

Pia katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, Wambura anadiawa kutenda kosa hilo, Juni 17, 2015 huko katika ofisi za TFF, ambapo kwa njia ya udanganyifu, mshtakiwa alijipayia milioni 10 kutoka TFF kwa kuonesha kuwa ni malipo ya USD 30,000 pamoja na riba kutoka kwenye kampuni hiyo ha Jeck jambo ambalo siyo kweli.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wambura anadai, kati ya Agosti 15 na Oktoba 21, 2014, makao makuu ya Shirikisho hilo, alijipatia Sh milioni 25 kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

Shtaka lingine la utakatishaji fedha haramu, mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 2015, alijipatia Sh 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali na zimetokana na shtaka la kughushi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.