banner68
banner58

Mkwasa aipinga TFF, aendeleza msimamo wa kutoshiriki Kagame

TFF waitaka Yanga kubadili maamuzi, au wakabiliwe na adhabu kali

Mkwasa aipinga TFF, aendeleza msimamo wa kutoshiriki Kagame

TFF waitaka Yanga kubadili maamuzi, au wakabiliwe na adhabu kali

11 June 2018 Monday 11:02
Mkwasa aipinga TFF, aendeleza msimamo wa kutoshiriki Kagame

Na Mwandishi wetu

Mkwasa ameamua kuwagomea TFF kuhusu kucheza michuano ya Kagame baada ya kuomba kujitoa, huku shirikisho hilo la soka nchini likiwashushia mkwala mzito.

“Wachezaji wetu wapo likizo hivyo sio rahisi sisi kushiriki michuano hiyo, wanarudi June 25 watapata wapi nguvu? Pia mikataba ya wachezaji wetu imeisha. Walio nayo ni saba, hivyo tupo katika mazungunzo,” amesema

Juzi Karia alisikika akisema kuwa Yanga wanapaswa kukaa na kujitafakari upya kutokana na maamuzi yao akieleza kuwa hayana mashiko, na akiwapa saa 48 pekee kutengua maamuzi yao.

Kwa mujibu wa Mkwasa, amesema kuwa kikosi chao kina wachezaji 7 pekee walio na mikataba huku wengine wote akieleza kuwa hawajasaini mikataba na timu hiyo ya Jangwani, na hivyo itakuwa vigumu kwao kuweza kushiriki mashindano hayo yanayotaraji kuanza Juni 28.

Mbali na wachezaji kukosa mikataba, Mkwasa amesema pia wachezaji wao wa kikosi cha pili wanashiriki mashindano ya Uhai CUP hivyo hawatoweza kutumika mara mbili.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Hassan Ally Said 2018-06-11 11:34:13

Binafsi naona nijambo jema, kupumzika kutoshiriki
Ili pia yanga wawe na maandalizi mazuri ya Timu yao
Pia huwezi kumlainisha mtu ale kitu asicho kipenda
Yanga oyeeeeeeeee