banner68
banner58

Mo Dewji afanya kufuru nyingine ya fedha Msimbazi

Mo Dewji afanya kufuru nyingine ya fedha Msimbazi

15 August 2018 Wednesday 08:41
Mo Dewji afanya kufuru nyingine ya fedha Msimbazi

SI bado unakumbuka kuwa hivi karibuni Simba ilitua kutokea Uturuki ilikokuwa imeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya?

Sasa taarifa nyingine ni kuwa msimu ujao timu hiyo iliyo chini ya mwekezaji bilionea kijana Mohammed Dewji ‘Mo’ itasafiri kisasa zaidi.

Tangu Simba iwe chini ya Mo haina shida za kifedha kama ambazo ilikuwa ikizipata misimu miwili iliyopita.

Unaambiwa kuwa msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22, mwaka huu, safari nyingi za timu hiyo za kwenda mikoani kucheza mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Kombe la FA, usafiri utakaokuwa ukitumika zaidi ni wa ndege, kuliko wa basi.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa usafiri wa basi utatumika tu kwa safari fupi kama vile kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar lakini pia mkoani Tanga kucheza na Coastal Union.

Inadaiwa kuwa uongozi wa timu hiyo umefikia hatua hiyo ili kupunguza hali ya uchovu kwa wachezaji wao ambayo wanaweza kukumbana nayo, pindi watakapokuwa wakisafiri kwa muda mrefu kwa kutumia usafiri wa basi.

“Kwa hiyo, msimu huu mambo ndivyo hivyo yatakavyokuwa na uongozi umejipanga vilivyo kwa hilo, kwa hiyo wachezaji safari hii wasituangushe na hatutaki visingizio kuwa wamechoka kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu kwa kutumia basi.

“Usafiri huo wa ndege wanatarajia kuanza kuutumia kesho (leo) ambapo wataondoka Dar es Salaam na kwenda Arusha kwa ajili ya kambi ya siku chache tu ya kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar itakayo

fanyika Agosti 18, mwaka huu huko jijini Mwanza,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Simba imerejea jana Jumapili kutoka Lindi ilikokuwa imeenda kucheza mechi ya kirafiki ya uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa ulioko Kiwangwa ambao umeitwa kwa heshima ya jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Iddi Kajuna, alisema kuwa wamejipanga kwa hilo na watatumia njia zote mbili za usafiri pale itakapobidi kufanya hivyo.

“Hiyo ni kweli kwani tumejipanga kwa hilo, ila tutatumia usafiri wa ndege na basi pale tutakapoona inafaa kutumia moja ya usafiri huo kwa ajili ya safari zetu,” alisema Kajuna.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Steven ezekiel 2018-08-15 11:35:13

Hiyo nimeipenda sana na pia itasaidia timu yetu kutokuwa na uchovu mwingi ila ni waambie tu timu yetu isituangushe sisi wapenzi wao

Avatar
Selemani Mustapha 2018-08-16 00:10:10

Simba nguvu moja watapata tabu sana

Avatar
Jeremiah kihingullah 2018-09-02 19:23:12

Wataelewa tu kwa miaka ya nyuma tulipata shida sana na walitucheka sana jirani zetu watakuwa wanatuona tu.

Avatar
sadala f simba 2018-09-05 16:30:46

MBONA MTAKOMA MWAKA HUU NA SIO TU MWAKA HUU HII NI MPAKA MAL 5

Avatar
ANAFI FURAHA 2018-09-13 20:45:30

Naipenda simba naninawa takia kila laheri

Avatar
SYLVESTER MKUCHU 2018-09-14 11:17:10

Hii ndo simba ninayo ijua mm najiona nimekamilika kuchagua simba

Avatar
saidi chembe 2018-10-12 08:19:28

Mo dewji Jana ilikuweje kawaida mi changamoto katika maixha

Avatar
saidi chembe 2018-10-12 08:19:45

Mo dewji Jana ilikuweje kawaida mi changamoto katika maixha