banner68
banner58

Mo Dewji akubali hisa asilimia 49 Simba

Mkutano mkuu kufanyika Mei 19 mwaka huu kufanya mabadiliko hayo makubwa

banner57

Mo Dewji akubali hisa asilimia 49 Simba

Mkutano mkuu kufanyika Mei 19 mwaka huu kufanya mabadiliko hayo makubwa

16 May 2018 Wednesday 18:26
Mo Dewji akubali hisa asilimia 49 Simba

Mabingwa wa Soka nchini Tanzania, klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, imetangaza kufanya mkutano wa kihistoria ambao utakuja na mabadiliko makubwa ndani ya klabu hiyo yatakayowawezesha wanachama kuwa na mamlaka zaidi kuliko muwekezaji katika klabu hiyo.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Simba, Haji Manara, alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mchana wa leo, ambapo amesema kuwa endapo mapendekezo ya mabadiliko yatapitishwa, basi klabu hiyo inaweza kuwa na mafanikio zaidi, na kuwa klabu ya mfano barani Afrika.

“Mabadiliko hayo yatawapa mamlaka wanachama waliowekeza ndani ya klabu umiliki wa timu kwa asilimia 51 na asilimia 49 zitachukuliwa na muwekezaji mkuu, mabadiliko haya yanakwenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta yetu ya michezo Tanzania na hata Afrika Mashariki”, amesema Manara.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Klabu ya Simba, Evodius Mtawala, amesema taratibu zote zimefuatwa na kinachosubiriwa sasa ni siku hiyo ya Jumapili ifike, ambapo amesema wanakwenda kufanya mabadiliko ya kikatiba, na hivyo kuwataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo.

Aidha, katika hatua nyingine, Manara amewaahidi watanzania kupata burudani safi kutoka kwa timu yao ya Simba katika mtanange wao na Kagera Sugar, siku ya Jumamosi Mei 19, mchezo ambao timu ya Simba inatarajia kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu Bara (VPL).

DarMpya

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.