Mo Salah awapiku Messi, Ronaldo Ulaya

Salah ambaye amefunga magoli 31 ya ligi kuu England maarufu kama ‘EPL’

Mo Salah awapiku Messi, Ronaldo Ulaya

Salah ambaye amefunga magoli 31 ya ligi kuu England maarufu kama ‘EPL’

25 April 2018 Wednesday 13:42
Mo Salah awapiku Messi, Ronaldo Ulaya

Na Amini Nyaungo

Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ndiye mfungaji bora mwenye magoli mengi Barani Ulaya baada ya jana kufunga magoli 2 na kufikisha idadi ya magoli 43 bao moja zaidi ya Cristiano Ronaldo na matatu zaidi ya Lionel Messi.

Salah ambaye amefunga magoli 31 ya ligi kuu England maarufu kama ‘EPL’ pamoja na magoli 12 mashindano mengine ya Barani humo.

Nyota huyo ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya England siku ya jumamosi, usiku wa jana ameisaidia timu ya yake ya Liverpool kushinda magoli 5-2.

Salah amewashinda wachezaji nyota duniani Cristiano Ronaldo ambaye amefunga magoli 42 huku Ciro Immobile akifunga magoli 41 akifuatiwa na Lionel Messi mwenye magoli 40, huku Robert Lewandowski akifunga magoli 39.

Mohamedi salah ni mchezaji wa kwanza kutoka Africa kufikisha magoli mengi Zaidi ikiwa bado msimu haujaisha.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
sure man 2018-10-14 16:23:42

mo salaa are good prayer on Europe