banner68
banner58

Mohamed Dewji ampigia simu Try Again nchini Cape Verde

Mohamed Dewji ampigia simu Try Again nchini Cape Verde

11 October 2018 Thursday 15:45
Mohamed Dewji ampigia simu Try Again nchini Cape Verde

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kutulia baada ya tukio la mwanachama mwenzao, Mohammed Dewji 'Mo' kutekwa na ameweka wazi kuwa alimpigia simu kabla ya tukio.

Try Again ni miongoni mwa wadau waliokwenda nchini Cape Verde kwa ajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa Stars.

Alisema, tukio hilo ni la kusikitisha na amewaomba Watanzania hususani wanachama wa Simba watulie.

"Jambo linalotakiwa kufanywa sasa ni kumwombea dua, ili mwenzetu awe salama huko alipo na jeshi la polisi linafuatilia kwa ukaribu suala hilo," alisema Try Again.

Amefafanua kuwa, jana Jumatano, Mo alimpigia simu kuomba mawazo kwake na wakaongea kwa kipindi kirefu.

"Alikuwa na kikao cha bodi na kuna mambo aliomba nimshauri, lakini ndiyo hivyo tena," alifafanua.

Namna alivyowatuliza wachezaji wa Simba ambao wako na Taifa Stars nchini Cape Verde.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.