Mrithi wa Yanga amepatikana Kagame

Ni timu kutoka nchini Uganda

Mrithi wa Yanga amepatikana Kagame

Ni timu kutoka nchini Uganda

15 June 2018 Friday 12:05
Mrithi wa Yanga amepatikana Kagame

Shirikisho la soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) limekubali ombi la klabu ya Yanga kujitoa kushiriki michuano ya Kagame Cup na sasa nafasi yao wamepewa mabingwa wa ligi kuu ya Uganda Azam Premier League timu ya Vipers Sc.

Klabu ya Yanga Sc iliyokuwa kundi C iliandika barua kwenda CECAFA kuomba kujitoa kwa sababu wachezaji wao wengi kutokuwa na mikataba pia kubanwa na ratiba ya mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia July 18.

Kwa maana hiyo, Vipers Sc ya Uganda wataingia kundi C na kuwa na timu za Simba Sc ya Tanzania, St George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.

Vipers Sc wataanza mechi ya kwanza na timu ya St George June 29 huku mchezo wa pili watacheza na Dakadaha July 02 na kumaliza na Simba July 5.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.