banner68
banner58

Msuva kuiona klabu Bingwa Afrika katika TV

Difaa El Jadida imemaliza ikiwa na nafasi ya tano ikikusanya alama 48

Msuva kuiona klabu Bingwa Afrika katika TV

Difaa El Jadida imemaliza ikiwa na nafasi ya tano ikikusanya alama 48

22 May 2018 Tuesday 12:15
Msuva kuiona klabu Bingwa Afrika katika TV

Na Amini Nyaungo

Licha ya kuisaidia timu yake kupata ushindi hapo jana na kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya Morocco maarufu kama Batola League sasa msimu ujao atakosa kushiriki michuano mikubwa barani Afrika.

Difaa El Jadida imemaliza ikiwa na nafasi ya tano ikikusanya alama 48 hivyo itashindwa kupata nafasi ya kuiwakilisha Morocco katika michuano ya Klabu Bingwa au mashindano hayo hapo mwakani.

Kwa sasa timu hiyo ipo katika hatua ya makundi ikiwa pamoja na TP Mazembe ya nchini DRC ambapo wiki iliyopita iliambulia kipigo.

Tumaini pekee la kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika ni kufanya vizuri na kufanikisha kampeni yake ya kuchukua ubingwa huo ambao timu hiyo inashiriki vinginevyo atabaki kutazama kwenye televisheni mwakani.

Msuva ameweza kufanya vizuri baada ya kujiunga na timu hiyo mwaka uliopita akitokea kwa Mabingwa wa zamani wa Tanzania Yanga Juni 30.

Ameweza kufunga magoli 11 ya ligi hiyo huku akifunga magoli 5 ya ligi ya Mabingwa na akifunga magoli 13 ya mechi za kirafiki.

Msuva amefunga magoli 4 ya timu ya taifa ya Tanzania hivyo jumla amefunga magoli 31.

Ndoto za mchezaji huyo za kuelekea Ulaya zinaweza kutimia endapo ataongeza jitihada kwani tayari hata thamani yake imekuwa kuwa endapo timu inahitaji huduma yake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Rajaman 2018-05-22 19:40:07

Soloo