banner58

Mtibwa sugar mabingwa Kombe la FA, je wataiwakilisha nchi Afrika?

Mabingwa wa Kombe la FA huiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa Afrika

Mtibwa sugar mabingwa Kombe la FA, je wataiwakilisha nchi Afrika?

Mabingwa wa Kombe la FA huiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa Afrika

02 June 2018 Saturday 17:19
Mtibwa sugar mabingwa Kombe la FA, je wataiwakilisha nchi Afrika?

Na Amini Nyaungo

Singida United imekubali kipigo mbele ya vijana wa Mtibwa Sugar baada ya kukubali kipigo cha bao 3-2, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumamosi hii.

Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar wametawazwa kuwa mabingwa wa kombe la shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup, hivyo kujipatia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.

Mtibwa ilitangulia kupata goli kupitia kwa Salum Kihimbwa dakika ya 21 wakati la pili likiwekwa kimiani na Issa Rashid dakika ya 37, huku goli la kwanza la Singida United lilipatikana mnamo dakika ya 43 kupitia kwa mchezaji Salum Chuku.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku timu zote zikitaka ushindi na ndipo Tafadzwa Kutinyu alipoisawazishia Singida United na kufanya matokeo kuwa ya bao 2-2.

Katika dakika ya 80 Issa Rashid wa Mtibwa Sugar alipata kadi nyekundu hivyo kubakiwa na wachezaji 9 uwanjani.

Pamoja na kuwa pungufu, lakini Mtibwa ndiyo walioibuka na ushindi baada ya Ismael Kihesa kupeleka kilio huko mjini Singida baada ya kufunga bao la tatu kwenye dakika ya 87 ambalo lilidumu hadi mchezo huo unamalizika, na Mtibwa kuibuka kwa ushindi huo wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United.

Mfungaji bora ni Hassan Dilunga wa Mtibwa Sugar ambaye amefunga magoli 4 akiwa sawa na Tafadzwa Kutinyu Singida United.

Jambo kubwa ambalo washabiki wa soka nchini wamekuwa wakijiuliza ni juu ya ushiriki wa Mtibwa katika michuano barani Afrika baada ya kufungiwa kwa miaka na shirikisho la soka barani humo CAF.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.