banner68
banner58

Muda mfupi baada ya kusaini Singida United, Fei Toto atua Jangwani

Muda mfupi baada ya kusaini Singida United, Fei Toto atua Jangwani

12 July 2018 Thursday 17:59
Muda mfupi baada ya kusaini Singida United, Fei Toto atua Jangwani

Hatimaye kiungo Feisal Salum Abdalah “Fei Toto” ametambulishwa rasmi na uongozi wa klabu ya Yanga.

Fei Toto kutoka JKU amejiunga na Yanga akisaini mkataba wa miaka mitatu ikiwa ni saa chache baada ya kutangazwa amejiunga na Singida United.

Singida United kupitia Mkurugenzi wao, Festo Sanga, leo mchana walimtangaza Fei Toto kuwa amejiunga nao wakionyesha picha wakati anasaini na kukabidhiwa jezi za Singida United.

Lakini leo, Yanga imemtangaza rasmi kutua Jangwani huku ikielezwa mkataba wa Singida United ulikuwa na matatizo.

Baadaye wakasambaza video zikimuonyesha akieleza alivyojiunga na Singida United lakini hivi punde atatambulishwa Yanga.

Pamoja na Fei Toto alionekana akizungumzia kwenye video kueleza alivyotua Singida United na ataitumikia msimu ujao.

Updated: 12.07.2018 18:03
Keywords:
YangaFei Toto
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Ally Said 2018-07-12 18:40:10

Mnatuchanganya