Mwakyembe aweka jiwe uwanja wa Simba, Mo Dewji aingiza milioni 20

Mwakyembe aweka jiwe uwanja wa Simba, Mo Dewji aingiza milioni 20

05 August 2019 Monday 12:43
Mwakyembe aweka jiwe uwanja wa Simba, Mo Dewji aingiza milioni 20

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameweka rasmi jiwe la msingi wa ujenzi wa uwanja wa nyasi bandia na asilia eneo la  Bunju B, jijini Dar es Salaam. Uwanja huo unamilikiwa na klabu ya Simba

Akishuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo leo Agosti 5, 2019 pamoja na mambo mengine Mwakyembe amewataka waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja.

"Sasa wakati umefika, viongozi wa klabu ya Simba leteni mchanganuo wenu na jinsi mnavyopata fedha kwa ajili ya ujenzi wa huu uwanja ili Serikali ikibidi nayo itaangalia itakavyochangia na kuwahimiza wadau wengine'' amesema 

Awali mwenyekiti wa bodi ya Simba SC, Mohamed Dewji 'MO' ameahidi kutoa milioni 20 zitakazotumika katika ujenzi huo na kwamba itafanyika harambee kubwa ya kuchangia ujenzi  huo

"Ujenzi wa uwanja huu utakwenda kwa awamu, awamu ya kwanza nitatoa milioni 20 kufanikisha ujenzi huu,'' amesema MO

Awamu ya kwanza ya uwanja huo itakuwa ni uwekaji wa nyasi bandia na mwingine nyasi za asili. Pia inatarajiwa kuwepo majukwaa, hostel na  sehemu ya mazoezi ya viungo(Gym)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.