Mwigulu Mchemba ainyonga Yanga kama haijui

Ni katika mbio za usajili wa wachezaji zinazoendelea nchini kwa sasa

Mwigulu Mchemba ainyonga Yanga kama haijui

Ni katika mbio za usajili wa wachezaji zinazoendelea nchini kwa sasa

31 May 2018 Thursday 11:31
Mwigulu Mchemba ainyonga Yanga kama haijui

Na Amini Nyaungo

Wakati mwingine pesa ndiyo kila kitu. Msemo huu umethibitishwa baada ya klabu kongwe nchini Yanga kupokonywa mchezaji Tiber John wa Ndanda FC ambaye klabu hiyo ya Jangwani ilikuwa katika hatua za mwisho kuhakikisha kuwa inapata saini yake.

Mchongo uko hivi, Yanga walikuwa tayari wanamawasiliano mazuri na kinda huyo, baada ya ligi kuisha jumatatu nyota huyo aliondoka siku inayofuata kuelekea jijini Dar es Salaam kumalizana na Yanga.

Kilichotokea Temeke ndio kil kilichotokea kwa Ronaldinho wakati kila mmoja akiamini kwamba nyota huyo tayari ni kila kitu kinaonyesha kuwa atakuwa mchezaji wa Manchester United ndani ya masaa machache, Barcelona waliingia dakika za mwisho na kumtoa mikonono mwa Sir Alex Ferguson.

Na ndicho walichofanya Singida United kwa kumsubiri nyota huyo maeneo ya Temeke na kumwongezea dau ambalo linadaiwa kuwa shilingi milioni 40.

Katika harakati hizo Simba nao walikuwa karibu kumfuatilia na tetesi zinasema walipenyeza milioni 35, lakini mchezaji huyo alitaka milioni 40.

Inaarifiwa na vyanzo vya kuaminika kuwa Singida United watamtangaza muda wowote kuanzia hii leo huku wakisajili nyota wengine watatu.

Azania Post

Keywords:
Tiber John
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.