banner68
banner58

Mwinyi Zahera amkataa huyu ndani ya Yanga

Mwinyi Zahera amkataa huyu ndani ya Yanga

21 September 2018 Friday 07:44
Mwinyi Zahera amkataa huyu ndani ya Yanga

Katika kuonyesha kweli hataki utani kocha wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amesema hahitaji msaidizi mwingine zaidi ya Mzambia, Noel Mwandila sababu ameridhika na utendaji wake wa kazi na wanafanya kazi vizuri kwa kushirikiana.

Zahera alipowasili nchini kwa mara ya kwanza wengi walitarajia kocha huyo angekuja na msaidizi wake lakini haikuwa hivyo bali aliendelea kufanya kazi na kocha huyo ambaye alimkuta, ingawa alileta msaidizi mmoja kutoka DR Congo akaingia mitini baada ya kuona hapasomeki.

Alisema kuwa; “Kufanya kazi na kocha ambaye mnaelewana na kushirikiana vyema ni jambo zuri ndiyo maana mimi sina tatizo na Mwandila na sihitaji kuletewa kocha mwingine sababu tunafanya kazi yetu bila matatizo yoyote hata nisipok-uwepo huwa sina hofu sababu ni mtu makini.”

“Mwandila ni kocha ambaye ana uzoefu mzuri na anajua nini cha kufanya ili timu yake iweze kupambana kwa ufupi naweza kusema tu ni kocha mwenye uwezo mzuri.

“Na mimi kama kocha mkuu ndiye nina uwezo wa kusema kuwa nahitaji kufanya kazi na nani na hakuna wakunipangia hivyo hakuna nimechagua kufanya kazi na Mwandila na si mtu mwingine watambue na Yanga haina mpango wa kuleta kocha mwingine hilo liko wazi,” alisema Zahera ambaye kila akiondoka kwenda timu ya Taifa amekuwa akilalamika kwamba wachezaji wanatawanyika.

Updated: 21.09.2018 09:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Paul Charles 2018-09-22 10:53:52

You can use this space to write comments. Please keep in mind when writing a review of the written warning!