banner68
banner58

Mwinyi Zahera awashangaa wadau Yanga wanaobeza timu yake

Mwinyi Zahera awashangaa wadau Yanga wanaobeza timu yake

03 November 2018 Saturday 08:47
Mwinyi Zahera awashangaa wadau Yanga wanaobeza timu yake

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameibuka na kupingana na baadhi ya wadau wa soka wanaohoji kwanini timu yake haifungi mabao mengi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mechi kadhaa zilizopita kikosi cha Yanga kushindwa kufunga mabao mengi kwenye michezo yake.

Zahera amesema kuwa wao wanachokiangalia ni ushindi na kupata alama tatu pekee ili kujiwekea nafasi nzuri za kutwaa ubingwa.

Mkongomani huyo ameweka wazi kuwa ligi ni ngumu na ina mechi nyingi hivyo amewaasa wale wote wanaozungumzia mabao mengi ni vema wakazingatia alama tatu kwanza.

Yanga itakuwa kibaruani kesho kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Ndanda FC ya Mtwara.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.