Mzee Akilimali amshauri jambo Haji Manara

Mzee Akilimali amshauri jambo Haji Manara

16 September 2018 Sunday 07:49
Mzee Akilimali amshauri jambo Haji Manara

Baada ya kushindwa kutamba mbele ya Ndanda FC jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kutoka nayo suluhu ya kutofungana, Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amemtaka Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kupunguza maneno.

Akilimali ameibuka na kumpa pole Manara akisema kuwa ni mdogo wake na hawezi sana kumtania japo amemuomba kupunguza zaidi maneno kuliko vitendo.

Mze huyo kwa busara kabisa amemtaka Manara kupunguza zaidi tambo za kujigamba na badala yake amemuelewesha kuwa kwenye huwa kuna aina ya matokeo matatu.

Katibu huyo wa Baraza la Wazee ameeleza kuwa Manara amekuwa akiwatania zaidi Yanga huku akiipa sifa kubwa Simba na kusahau kama mpira huwa na matokeo ya aina yake.

Mzee huyo anaamini suluhu waliyoipata Simba dhidi ya Ndanda itakuwa imewapa funzo kuwa hii ndiyo na kila mechi inakuwa na changamoto zake.

"Unajua huyu mdogo wangu nadhani bado hajaitambua ligi vizuri, namshauri tu vizuri kwa maana siwezi kumtania ni vema akaelewa kuwa mchezo una matokeo matatu. Namuomba apunguze zaidi tambo kwa timu yake na atambue kuwa si kila mechi unaweza kushinda" alisema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.