Namungo FC wamnasa Paul Ngalema

Namungo FC wamnasa Paul Ngalema

19 June 2019 Wednesday 08:38
Namungo FC wamnasa Paul Ngalema

Na Oliver Albert, Dar es Salaam
Namungo FC imeendelea kujiimarisha kwenye kikosi chake baada ya kumnasa beki wa kushoto  kutoka Lipuli FC ya Iringa, Paul Ngalema.

Namungo imepanda daraja na itacheza Ligi Kuu Bara kwa mara ya Kwanza msimu 2019/20.

Timu hiyo ya Ruangwa Lindi imeonekana itakuja kuwa tishio kwani imekuwa ikifanya usajili mzuri kwa ajili ya kujiimarisha na Ligi msimu ujao.

Pia tayari ilimsajili mshambuliji wa zamani wa Stand United na Alliance FC,Bigirimana Blaise kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Pia Namungo imewaongezea mkataba wachezaji wake watatu Reliants Lusajo, Daniel Joram na Jukumu Kibanda ili kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha wa zamani wa Biashara United na  raia wa Burundi Hitimana Thierry kilipanda daraja mwaka huu 2019 pamoja na Polisi Tanzania.

Updated: 19.06.2019 11:46
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.