Nini Mo Salah, Samatta apagawisha mbaya

Nini Mo Salah, Samatta apagawisha mbaya

01 September 2018 Saturday 16:28
Nini Mo Salah, Samatta apagawisha mbaya

SHOO za kibabe za mshambuliaji, Mohamed Salah msimu uliopita wa 2017/18  ziliwafanya mashabiki wa Liverpool kutunga na kumwimbia wimbo nyota huyo mwenye uwezo wa kutumia zaidi mguu wa kushoto.

Salah aliimbiwa wimbo huo pindi  ambapo Liverpool ilipotoa dozi  kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield ya mabao  4-3  dhidi ya Manchester City, Januari 14, 2018.

Mfungaji bora huyo  wa Ligi Kuu England, aliimbiwa wimbo huo  kwa kutajwa jina lake  ‘Mo Salah, Mo Salah’ na wakaingizia maneno yenye maana ya kuwa anauwezo wa kukimbiza kwenye winga ‘Salah la la la la la la la’ na mwisho wakamtaja kuwa ni mfalme wa Misri.

Wakati mashabiki wa Liverpool wakifanya hivyo kwa Salah, unaambia Wabelgiji nao wameliamsha dude, wamekuja na mpya kwa kuanza kumwimbia wimbo mshambuliaji wa kutegemewa wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.

Samatta amekuwa kipenzi cha mashabiki wa KRC Genk kutokana na kiwango anachoendelea kukionyesha msimu huu wa 2018/19 ambapo tayari ameshaifanya timu hiyo kutinga kwenye makundi ya Kombe la Europa Ligi.

Mashabiki hao wamesikika kwenye michezo kadhaa ya hivi karibuni ya KRC Genk ukiwemo ule aliyepachika mabao matatu ‘hat trick’ dhidi ya Brondby IF wakiimba ‘Samagoal, Samagoal, Sama…Sama goal lalaaaa.

Samatta anatarajiwa kutua nchini kabla ya Jumanne kujiunga na wachezaji wenzake wa Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kuwania tiketi ya Afcon mwakani nchini Cameroon kwa kucheza ugenini dhidi ya Uganda, Septemba 8.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.