Nsajigwa akubali yaishe, aachia ngazi Yanga

Nsajigwa ni beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, na alikuwa mchezaji mwenye mafanikio sana

Nsajigwa akubali yaishe, aachia ngazi Yanga

Nsajigwa ni beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, na alikuwa mchezaji mwenye mafanikio sana

05 June 2018 Tuesday 11:57
Nsajigwa akubali yaishe, aachia ngazi Yanga

Na Amini Nyaungo

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa leo hii ameachia ngazi baada ya kumaliza mkataba wake kwa timu hiyo ya maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Nsajigwa ameona isiwe taabu baada ya kupokea maneno mazito kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa hafai na hapo ndipo alipoona aachie ngazi baada ya mkataba wake kumalizika.

“Nimemaliza mkataba wangu nimeamua kuodoka kama makocha wengine huwa wanavyofanya,” amesema.

Nsajigwa alikuwa kocha wa kikosi cha pili cha Yanga, kwa maana ya Yanga ‘B’ kabla ya kupandishwa na kuwa kocha msaidizi namba tatu wakati wa George Lwandamina.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.