banner68
banner58

Nyota huyu Yanga hatihati kuikosa Simba

Nyota huyu Yanga hatihati kuikosa Simba

24 September 2018 Monday 07:34
Nyota huyu Yanga hatihati kuikosa Simba

Yawezeka ikawa pengo na pigo kwa Yanga ambapo mchezaji wake aliyekuja kwa kasi, Mkongomani, Heritier Makambo yupo kwenye hatihati ya kuikosa mechi ya watani wa ajdi dhidi ya Simba.

Makambo hakuwepo kwenye kikosi cha jana kilichocheza dhidi ya Singida United na kufanikiwa kuibuka na mabao 2-0 dhidi ya Singida United.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema straika huyo alikuwa hayuko fiti licha ya kufanya mazoezi siku ya mwisho kuelekea mechi na Singida lakini jina lake likakosekana katika kikosi cha jana.

Katika mchezo huo, Mwinyi Zahera alimpa majukumu Amis Tambwe akichukua nafasi ya Makambo na kufanikiwa kutupia mabao mawili yakiwa ni ya ushindi dhidi ya Singida United.

Licha ya kuikosa Singida, inaelezwa pia hali ya mchezaji huyo si mbaya kiasi cha kwamba uwezekano wa kucheza dhidi ya Simba kwa asilimia kubwa, mechi ambayo itapigwa Septemba 30 2018.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.