Orodha kamili ya waliosajiliwa Simba hadi sasa hii hapa

Orodha kamili ya waliosajiliwa Simba hadi sasa hii hapa

28 June 2018 Thursday 14:21
Orodha kamili ya waliosajiliwa Simba hadi sasa hii hapa

Na Amini Nyaungo

Yale majina ambayo tulitoa taarifa asubuhi kuwa msemaji mkuu wa Simba Haji Manara atakuwa na kikao cha waandishi wa habari ili kutaja majina ya wachezaji wapya iko tayari.

Waliotambulishwa ni pamoja na Serge Wawa, Deogratius Munishi pamoja na Meddie Kagere wengine ni Adam Salamba, Mohamedi Rashid na Marcel Kaheza ambao walisajiliwa mapema wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.

Wachezaji ambao wamethibitishwa kuwa wamesaini mikataba mipya ni pamoja na Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya na Mzamiru Yassini.

Haji Manara amesema kuwa bado wanaendelea na usajili hivyo wasubiri vitu vingi vinakuja.

“Tunaendelea na usajili bado hatujamaliza yoyote atakayopendekezwa na benchi la ufundi tutamsajili,” amesema Manara.

Manara pia ametoa sababu ya kusajili wachezaji wengi katika nafasi moja, ikiwemo nafasi ya goli kipa pamoja na washambuliaji ambapo wapo wanne katika idara hizo.

“Ni kweli tumesajili wachezaji wengi, hatutaki itokee ile ya msimu uliopita kabla ya huu, tulikosa ubingwa sababu ya magoli, pia tuna mashindano mengi lazima tuwe na wachezaji wengi kikosini,” amesema.

Neno la kocha Masudi Djuma

Kwa upande wake amesema anawapa wachezaji wote nafasi kama alivyoingia wengi waliona namna alivyowatumia wachezaji ambao hawapati nafasi na atafanya hivyo kwa kipindi cha mbele.

Amewaambia wote wanaosema wamesajili wachezaji wazee, anataka wabadilishe kauli hiyo waseme wamesajili wachezaji wa kazi.

“Watu wazee ni wazazi wao ambao wako nyumbani, hawa ni watu wa kazi,” amesema.

Timu hiyo ambayo inajiandaa na michuano ya Kagame tayari imesajili nyota kama Adam Salamba, Marcel Kaheza, Serge Wawa, Deogratius Munishi na Medie Kagere.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Aleld frasnceco 2018-08-08 21:45:32

Simba ya mwaka huu achaa,kama huna nguvu pita mbali nayo.

Avatar
Juventus 2018-09-04 10:42:18

tunawaomba wachezaji wasimba waji2me uwanjan tuweze kuchukua ubingwa tena mungu ibarik simba amina SIMBA NGUVU MOJA!!

Avatar
Luhende njile wa katavi 2018-07-28 21:21:14

Simba moto wakuotea mbali hatari sana!!!

Avatar
Packsence charles 2018-08-03 21:35:50

Simba tunataka kuchukua ubingwa tena 2018-2019

Avatar
Shukuru sungura wa mbwewe pwani 2018-08-06 16:16:08

Simba bingwa tena,ubingwa raha

Avatar
HAMMIE ZE SAINT 2018-08-08 15:32:13

DAA-kwanza leo simba day iko amazing sana kinyama-so salute kwao wana#Red-Lion-ze king

Avatar
Watxon Mwang'amba 2018-09-11 23:37:58

Kwasasa Simba Tuko Vizuri, Kubwa Ni Kwamba Wachezaji Wanatakiwa Watambue Zaidi Fursa Walio Nayo Ili Waweze Kufanya Vzr. Simba Damu

Avatar
bahath paul makoye 2018-09-14 20:47:30

wachezaji wa simba wajitume wasijione wanaweza sana