banner68
banner58

Patrick Aussems agomea nyumba Simba SC

Patrick Aussems agomea nyumba Simba SC

16 September 2018 Sunday 08:25
Patrick Aussems agomea nyumba Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa, anataka kuendelea kukaa hotelini kwa kuwa amezoea na pia hajui kupika.

Aussems leo Jumamosi ataiongoza timu hiyo kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa tatu kwake na wa kwanza wa ugenini katika ligi ya msimu huu.

Ikumbukwe, Mbelgiji huyo alifikia katika Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki kabla ya kuhamishiwa katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach mara baada ya kuanza kazi kwenye timu hiyo na japo hulipa chumba Sh 170,000 kwa siku.

Akizungumza na gazeti moja hivi karibuni, Aussems alisema hawezi kukubali kuishi kwenye nyumba za kupangiwa kwa kuwa maisha yake ya ukocha amekuwa akiishi hotelini.

“Kwa hapa ndiyo sehemu ambayo nitaendelea kuishi kwa muda wote, nilishawaambia viongozi na hilo wanalijua hivyo siwezi kwenda kuishi kwenye nyumba yoyote zaidi ya hapa.

“Unajua kwanza sijui kupika halafu maisha ya hotelini nimeyazoea tangu nimeanza kufanya kazi Afrika nimekuwa nikiishi hoteli sawa na hapa na uzuri huwa sichagui chakula ili mradi kiwe kitamu,” alisema Aussems.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Saimon 2018-09-16 10:35:03

Akakae tu kwenye hiyo nyumba kula awe anakula hotelini kwa hela yake asilete za kuleta hapa