Piga Uwa: Simba kumrudisha Peter Manyika Jr ‘Kwa Mbwebwe’

Piga Uwa: Simba kumrudisha Peter Manyika Jr ‘Kwa Mbwebwe’

16 June 2018 Saturday 15:37
Piga Uwa: Simba kumrudisha Peter Manyika Jr ‘Kwa Mbwebwe’

Na Mwandishi wetu

Simba wako mbioni kumrejesha aliyekuwa kipa namba mbili Manjika Jr baada ya kuona Emanuel Mseja hana kiwango cha kuridhisha.

Habari za uhakika kutoka katika klabu ya Simba na Singida zinaesema wanahitaji kuimairisha kikosi chao kuanzia kipa namba moja hadi namba tatu awe anaumahiri wa hali ya juu.

Kwa upande wa goli kipa huyo wa Singida United amesema kuwa anafurahia maisha yake ya sasa, licha ya mpira kuwa biashara kwake.

“Nafurahi kucheza Singida United muda wangu huu wakuonesha kipaji changu, japo mpira ni kazi yangu, ila kucheza kila wiki ndio kitu kizuri kwangu,” amenukuliwa akisema.

Wakati huo huo kipa namba tatu wa Simba Emanuel Mseja ameuomba uongozi umpatie muda wa mwaka mmoja wa kujiuliza, ili kuonesha kipaji chake huku akiomba apate nafasi katika kikosi cha kwanza.

Simba kwa sasa ina makipa watatu Aishi Manula ndiye namba moja huku Said Mohamed Nduda akiwa wapili akisaidiwa na Emanuel Mseja.

Azania Post

Updated: 16.06.2018 16:52
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.