Rais ampa shavu Ozil

Rais ampa shavu Ozil

09 June 2019 Sunday 09:43
Rais ampa shavu Ozil

RAIS wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan ameshiriki na kumsaidia  mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil kufunga ndoa na mpenziwe mjini Instabul Uturuki

Ozil, ambaye chimbuko lake ni Uturuki, alizua hisia kali alipopiga picha na rais wa Uturuki Erdogan kabla ya kombe la dunia mwaka 2018.

Baadaye alistaafu katika soka ya kimataifa , akidai ubaguzi wa rangi na kutoheshimiwa baada ya picha hizo kusambaa nchini Ujerumani.

Kiungo huyo wa Arsenal alimuoa mpenzi wake malkia wa urembo wa Uturuki Amine Gulse , katika hoteli moja ya kifahari karibu na kingo za mto Bosphorus.

Wanandoa hao walianza kuchumbiana 2017 na kutangaza kilichokuwa kikiendelea kati yao mwezi Juni 2018.

Ozil alitangaza mwezi Machi mwaka huu kwamba alimuomba rais Erdogan kuwa mshenga wake swala ambalo lilizua hisia kali nchini Ujerumani.

Helge Braun, waziri wa Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliambia gazeti la Bild kwamba ilikuwa uchungu sana kumuona Ozil akimchagua kiongozi kama huyo baada ya shutuma alizopata na rais huyo wa Uturuki mwaka uliopita.

Inaripotiwa kwamba ni nadra sana Erdogan kuhudhuria harusi nchini Uturuki hususan wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hatua yake ya kuhudhuria harusi ya Ozil inaajiri wakati ambapo uchaguzi wa marudio wa Meya unasubiriwa mjini Instanbul.

Matokeo ya awali yalionyesha kwamba mgombea wake wa chama cha APK alishindwa kwa kura chache hatua iliyopelekea uchaguzi huo kufutiliwa mbali na kuzua hisia kali za kimataifa.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.