banner68
banner58

Raphael Daudi na Emanuel Martin waipaisha Yanga

Wolaitta Ditcha ina mlima mrefu wa endapo itataka kupita hatua inayofuata

Raphael Daudi na Emanuel Martin waipaisha Yanga

Wolaitta Ditcha ina mlima mrefu wa endapo itataka kupita hatua inayofuata

07 April 2018 Saturday 18:38
Raphael Daudi na Emanuel Martin waipaisha Yanga

Na Amini Nyaungo

Yanga Africa wamejaribu kufuta makosa yao ya kutotumia vizuri uwanja wa nyumbani mara baada ya kuifunga Wolaitta Ditcha ya Ethiopia kwa jumla ya magoli 2-0 katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kiungo wa Yanga Raphael Daudi amefunga goli la kwanza sekunde ya 30 ya mchezo huo akiunganisha krosi iliyopigwa na mlinzi Mwinyi Haji.

Kipindi cha kwanza kimeisha Yanga ikiwa mbele kwa goli 1-0 ambalo limedumu hadi dakika ya 54 ambapo Emanuel Martin ameongeza goli la pili akiunganisha krosi ya Yusuph Mhilu na ubao kuwa magoli 2-0.

Wolaitta Ditcha ina mlima mrefu wa endapo itataka kupita hatua inayofuata inatakiwa iifunge Yanga mabao 3-0 hatua ya pili mchezo utakaochezwa nchini Ethiopia.

Kocha George Lwandamina ameamua kubadilisha mfumo uliozoeleka kwa kumrudisha nyuma Pius Buswita akicheza sambamba na Thabani Kamusoko. Ambapo mfumo huo umeonekana kuinufaisha Yanga siku hii ya leo.

Yanga wamemiliki mpira kwa 53% wakati wageni wamemiliki kwa 47% mchezo huo haukuwa na kadi yoyote.

Mashuti yaliyolenga  goli 6 wamepiga jumla ya mshauti 16 kwa Yanga huku wageni wamaepiga mashuti  10 yaliyolenga goli 6 yaliyoenda nje manne.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema wameshinda mchezo huo  mchezo unaofuata mgumu sana, kazi ngumu inayofuata ila anaamini watashinda.

"Tumepata magoli mawili nyumbani imekuwa heri kwetu, tunashurkuru kwani hiki ndicho tulichofanikiwa, naamini tutasonga katika hatua ya makundi japo nafasi ngumu sana," amesema

Golikipa wa timu hiyo Wolaitta Ditcha  Wondwosen Genermew amesema wataifunga Yanga mchezo ujao kwani walikuwa hawaifahamu timu hiyo hapo awali.

"Tutajitahidi  mchezo unaofuata tushinde na tutaenda hatua inayofuata, awali hatukujua Yanga namna gani wanacheza ila sasa wamewajua," amesema.

Azania Post

Updated: 07.04.2018 20:35
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.