Real Madrid yasitisha uhamisho wa Bale kuelekea China

Real Madrid yasitisha uhamisho wa Bale kuelekea China

29 July 2019 Monday 05:13
Real Madrid yasitisha uhamisho wa Bale kuelekea China

Madrid, Hispania

Real Madrid  imesimamisha uhamisho wa winga  wake Gareth Bale kuelekea China na sasa winga huyo wa Wales anatarajiwa kubakia klabuni hapo.

Sababu kubwa ya kuzuiliwa  ni kufuatia kuumia kwa mchezaji Marco Asensio  katika mechi za kirafiki na uenda asiwepo kiwanjani kwa msimu mzima akiuuguza majereha

Bale, 30, alitarajiwa kujiunga na klabu ya China Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kulipwa  paundi milioni 1 kwa wiki .

Wiki iliopita meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane alisema kuwa Bale alikuwa anakaribia kuondoka Madrid baada ya kiwango chake cha mchezo kutokuwa vizuri.

Zidane aliongezea kwamba kuondoka kwake kutakuwa vyema kwa kila mtu. Bale alijiunga na miamba hiyo ya Uhispania kwa dau lililovunja rekodi la paundi milioni 85 kutoka Tottenham 2013.

Amebakia  na kandarasi ya miaka mitatu katika uwanja wa Bernabeu ambapo ameshinda mataji manne ya ligi ya mabingwa Ulaya , taji moja la la Liga, mataji matatu ya Uefa na mataji matatu ya klabu bora duniani.

Alifunga magoli matatu , pamoja na penalti katika fainali nne za ligi ya mabingwa baada ya kushinda kombe hilo 2014, 2016, 2017 and 2018.

Hatahivyo majeraha yamemkwaza kuanzishwa mara 79 katika misimu yote minne akiichezea R Madrid.

Aliichezea Real mechi 42 msimu uliopita lakini alizomelewa na mashabiki wa nyumbani katika mechi kadhaa .

Kurudi kwa Zidane katika timu hiyo kulidaiwa kuwa habari mbaya na ajenti wa mshambuliaji huyo Jonathan Barnett, kwa kuwa raia huyo wa Ufaransa hakutaka kufanya kazi na Bale na wawili hao walitofautiana kuhusu mfumo wa kucheza.

Bale alimaliza msimu uliopita kama mchezaji wa ziada wakati Real Madrid ilIpoandikisha matokeo mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 20 wakishindwa mara 12 na kupata pointi 68 na kuwa katika nafasi ya tatu - pointi 19 nyuma ya mabingwa Barcelona.

Updated: 29.07.2019 05:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.