Rekodi kombe la dunia: Ronaldo na Messi mbivu na mbichi kujulikana leo

Rekodi kombe la dunia: Ronaldo na Messi mbivu na mbichi kujulikana leo

30 June 2018 Saturday 12:22
Rekodi kombe la dunia: Ronaldo na Messi mbivu na mbichi kujulikana leo

Na Amini Nyaungo

Leo tunaingia hatua ya 16 bora ambapo hakuna timu yoyote kutoka Afrika iliyofanikiwa kuingia katika hatua hiyo ambayo imevunja rekodi yake ya miaka 16 mwaka huu haijaingia hatua hiyo.

Leo kuna mitanange ya kufa mtu ambapo mechi ya mapema Argetina na Ufaransa, Messi kuendelea hatua ya nane bora au safari kuisha leo, pia saa tatu usiku naye Ronaldo itafahamika kama ataendelea au safari yake inaishia leo.

Mechi ya saa 11 jioni Argentina dhidi ya Ufaransa ambapo tiketi tayari zishauzwa yaani zimejaa, huku saa tatu usiku Uruguay dhidi ya Ureno pia tiketi zimeisha tayari.

Rekodi mbalimbali za kombe la dunia kutokea hatua ya makundi

Magoli 122 yamefungwa katika hatua hiyo huku timu za Afrika zikifungwa magoli 25 na magoli 10 yamefungwa dakika 15 za mwisho na ndiyo wamezitoa timu za Afrika.

Kadi 158 za njano huku kadi nyekundu zikiwa tatu tu zimetolewa pasi 36,349 zimepigwa kwa usahihi huku Hispania ikipiga pasi 2089, Ujerumani wameshambulia mara 252 huku Iran wakiwa na timu bora iliyozuia hatari nyingi mara 149.

Harry Kane ndiye kinara wa ufungaji wa mabao akiwa amefunga magoli 5 akifuatiwa na Ronaldo na Lukaku amefunga magoli 4 nyota wa Urusi Denis Cheryshev akiweka mabao 3 sawa na Diego Costa wa Hispania.

Toni Kroos wa Ujerumani ndiye aliyepiga pasi nyingi mara 310 huku Eriksen wa Dernmark akikimbia kilomita 36.

Mechi ya Ubelgiji ndiye iliyozaa mabao mengi jumla mabao 7, nyota mwenye gharama kubwa duniani Neymar amefunga goli 1 katika hatua ya makundi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.