banner58

Rekodi mbovu kwa Yanga msimu huu

Zifuatazo ni rekodi mbovu kabisa za Yanga katika michuano yote msimu huu kutoka ligi kuu bara hadi kombe la shirikisho

Rekodi mbovu kwa Yanga msimu huu

Zifuatazo ni rekodi mbovu kabisa za Yanga katika michuano yote msimu huu kutoka ligi kuu bara hadi kombe la shirikisho

04 June 2018 Monday 12:04
Rekodi mbovu kwa Yanga msimu huu

Na Amini Nyaungo

Baada ya vipigo vya mara kwa mara kwa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, baadhi ya viongozi wake wanaonekana kujiweka pembeni, akiwemo Salum Mkemi.

Kaimu Mwenyekiti wa timu hyio Clement Sanga anaonekana hayupo na matumaini na timu hiyo baada ya kutoshughulika na mambo ya timu hiyo kwa muda mrefu sasa.

Huenda asiendelee na nafasi yake baada ya mkutano mkuu wa wanachama wa Yanga utakaofanyika Juni 10 jijini Dar es Salaam. Hii ni baada ya maelezo yake leo ambayo ameweka wazi kwamba zinatakiwa zijazwe nafasi zilizo wazi ikiwemo ya makamu mwenyekiti ambayo ndiyo nafasi yake na ile ya Mwenyekiti.

“Tutaongea mengi siku ya mkutano mkuu, inatakiwa nafasi ya mwenyekiti na makamu zijazwe katika mchakato huo,” amesema.

Zifuatazo ni rekodi mbovu kabisa za Yanga katika michuano yote msimu huu kutoka ligi kuu bara hadi kombe la shirikisho kuanzia Aprili 11.

Aprili 11, 2018; Yanga 1-1 Singida United (Ligi Kuu Dar es Salaam)

Aprili 18, 2018; Welayta Dicha 1-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho)

Aprili 22, 2018; Mbeya City 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya)

Aprili 29, 2018; Simba 1 – 0 Yanga SC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

Mei 6, 2018; USM Alger 4-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho Algiers)

Mei 10, 2018; Tanzania Prisons 2-0 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya)

Mei 13; 2018; Mtibwa Sugar 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu Morogoro)

Mei 16, 2018; Yanga SC 0-0 Rayon Sports (Kombe la Shirikisho Dar es Salaam)

Mei 19, 2018; Yanga SC 0-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)

Mei 22, 2018; Yanga SC 1-0 Mbao FC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

Mei 25, 2018; Yanga SC 2-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Dar es Salaam)

Mei 28, 2018; Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

Juni 3, 2018; Yanga SC 1-3 Kakamega Homeboys (SportPesa Super Cup)

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.