Ronaldo aitaka rekodi mpya, yajue haya baina ya Real Madrid na Bayern Munich

Yajue haya kabla ya mchezo huo wa leo usiku

Ronaldo aitaka rekodi mpya, yajue haya baina ya Real Madrid na Bayern Munich

Yajue haya kabla ya mchezo huo wa leo usiku

01 May 2018 Tuesday 12:45
Ronaldo aitaka rekodi mpya, yajue haya baina ya Real Madrid na Bayern Munich

Na Amini Nyaungo

Mchezo wa marudiano michuano ya Ulaya maarufu kama ‘UEFA Champion League’, Real Madrid watawakaribisha Bayern Munich katika uwanja wa Santiago Bernabeu usiku wa 9:45 leo jumanne.

Muamuzi wa mchezo huo Cuneyt Cakir abaye ni mzaliwa wa Jiji la Istanbul nchini Uturuki na kwa sasa anafanya vizuri akiwa na uwezo kubwa wa kuchezesha michezo mikubwa, ikiwemo ya fainali ya michuano hii hata ya kombe la Dunia.

Yajue haya kabla ya mchezo huo wa leo usiku

Cristiano Ronaldo amefunga magoli 8 dhidi ya Bayern Munich, Ronaldo ameweka rekodi ya kuifunga magoli mengi Juventus, magoli 10 hakuna mchezaji yoyote aliyefanya hivi katika michuano hii.

Leo anataka afunge magoli zaidi afikie rekodi yake yeye mwenyewe ya ufungaji wa mabao 16 katika msimu mmoja.

Hii ni mara ya 26 wanakutana wanakutana miamba hawa katika michuano ya Ulaya, Madrid wameshinda mara 12 wakati Bayern Munich wameshinda mara 11 na kutoa sare 2.

Bayern Munich wamepoteza michezo sita ya hivi karibu walipokutana na Real Madrid katika hatua mbalimbali za mtuano ya michuano hii.

Mara ya mwisho Bayern Munich kushinda ugenini dhidi ya Real Madrid ilikuwa mwaka 2001 ambapo matokeo yalikuwa 1-0 goli lililofungwa na Giovane Elber.

Real Madrid wamefunga magoli mengi katika michezo 41 waliyocheza katika dimba la Santiago Bernabeu katika michuano hii.

Chini ya Zinedine Zidane timu hiyo inayoongozwa na Rais Perez haijawahi kutolewa katika michuano hiyo.

Robert Lewandowski ameshindwa kufunga katika michezo minne ya michuano hii ya UEFA Champions League.

Rekodi za kuanzia msimu wa mwaka 2010 hdi 2018 Real Madrid imeshinda mara 7 wakati Bayern Munich imeshinda mara 2 ikitoka sare mara moja.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.