Sababu ya Mbenini Marcellin Koukpo kuondoka Zahera achangia

Sababu ya Mbenini Marcellin Koukpo kuondoka Zahera achangia

30 June 2018 Saturday 11:02
Sababu ya Mbenini Marcellin Koukpo kuondoka Zahera achangia

Na Amini Nyaungo

Baada ya jana Azania Post kuwa wa kwanza kuripoti habari ya kuondoka nyota wa Yanga aliyekuja kufanya majaribio Mercellin Koukpo na mchezaji huyo kuandika waraka mzito kuhusu soka la Tanzania, huku baadhi ya makundi ya Yanga ya facebook yakilalamika kwanini waandishi wa habari huifuatilia Yanga wakati kazi ya waandishi ni kutoa habari.

Sasa sababu ya kukimbia klabu hapo jana imejulikana, kuwa inawezekana kile alichokisema yeye kuwa kuna watu wa kati (yaani madalali) amewaita ‘middle men’ ndio wanaharibu soka la Tanzania ila upande wapili wa nao umesema yake.

Tatizo la kuondoka kwa nyota huyo

Siku tatu nyuma kupitia hapa Azania Post tulisema kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera aliwapa tizi la kufa mtu kama dakika 40, katika tizi hilo yeye amechemka katika kundi lake akawa mtu wa mwisho kukimbia.

Alionekana mzito sana na hakuwa fiti kuweza kuungana na Yanga ambayo ina kiu ya mafanikio huku ikielekea michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Gor Mahia mwezi ujao.

Mchezaji huyo alikuja nchini akijua kuwa hakuna majaribio yeye ni wakupita moja kwa moja, huku akipitia vipimo vya afya kabla kocha Zahera hajarejea nchini na dau lake la usajili likiripotiwa kuwa ni shilingi milioni 23.

Baada ya kuchemka tizi mchezaji huyo siku iliyofuata ambayo ni Ijumaa hakuweza kurejea tena mazoezini, kumbe alijua mzigo mzito hivyo kufanya uamuzi wa kufungasha virago na kuondoka nchini, na kuandika maneno mazito juu ya soka la Tanzania.

Lakini ukweli ni kwamba, ameshindwa kuucheza muziki wa Mkongomani Mwinyi Zahera hivyo kuamua kuondoka wala si kitu kingine na hakuna kiongozi aliye mwambia aondoke yeye mwenyewe amejiondoa.

Baada ya kusikia maneno hayo kocha Zahera amewaambia viongozi wa Yanga kuwa kuna wachezaji wawili tu wanaoweza kwenda popote bila kujaribiwa ila hawa wa Afrika lazima wajaribiwe.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.