banner68
banner58

Sababu za Banka kusajiliwa Yanga hizi hapa

Sababu za Banka kusajiliwa Yanga hizi hapa

11 July 2018 Wednesday 08:23
Sababu za Banka kusajiliwa Yanga hizi hapa

Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuhusiana na usajili wa kiungo mshambuliaji, Issa Mohammed Banka aliyetia kandarasi ya miaka miwili na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa mchezaji huyo waliyemsajili kutokea Mtibwa Sugar amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Uwanja.

Nyika ameeeleza kuwa hakuna asiyejua mchango wa Banka kutokana na umahili wake wa kutandaza soka kuwalisha mipira washambuliaji wa mwisho, kitu ambacho kimepelekea wao kumsajili.

Aidha, Nyika anaimani Banka atakuwa msaada ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinajiandaa hivi sasa kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Kuelekea mechi hiyo kubwa ya mkondo wa kwanza, Yanga itasafiri kwenda kuanzia Kenya ambapo itacheza dhidi ya mabingwa hao watetezi jijini Nairobi Julai 18 2018.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
costantine mikanda 2018-08-04 20:33:54

yanga hakuna kitu na moharmed banka wen mtalia2 kwa mnyama yuko vzr zaid yenu!!!

Avatar
Jimmy Yanga 2018-08-17 10:08:36

Yanga ndo baba wa soka TANZANIA NA AFRICA MASHARIKI

Avatar
Dende Edward 2018-08-17 15:10:55

kalibt jangwani