Salamba wa Simba kujaribiwa leo dhidi ya Kakamega Homeboys

Adam Salamba amesajiliwa hivi karibuni na Simba akitokea Lipuli FC ya Iringa

Salamba wa Simba kujaribiwa leo dhidi ya Kakamega Homeboys

Adam Salamba amesajiliwa hivi karibuni na Simba akitokea Lipuli FC ya Iringa

07 June 2018 Thursday 11:37
Salamba wa Simba kujaribiwa leo dhidi ya Kakamega Homeboys

Na Mwandishi wetu

Simba imeamua kuongeza nguvu kwa katika kikosi kinachoshiriki mashindano ya SportsPesa Super Cup huko jijini Nakuru nchini Kenya, baada ya kukiongezea nguvu kwa kumpeleka mshambuliaji wake mpya Adam Salamba kucheza dhidi ya Kakamega Home boys katika mchezo wa nusu fainali.

Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Masoud Juma amesema kwamba kutokana na ukubwa wa mashindano haya na kwa kuwa Salamba tayari ni mchezaji halali wa klabu hiyo wameona ni vyema aje aongeze nguvu katika kikosi cha timu hiyo ambacho leo kinashuka dimbani kumenyana na Kakamega.

"Ni kweli Adam Salamba amekwishafika nchini Kenya kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chetu kwa sababu tayari ni mchezaji halali wa klabu yetu, hivyo tumeona ni vizuri aje kutia nguvu katika mashindano haya ya SportSpesa Super Cup," amesema Masoud Juma.

Nusu Fainali za SportPesa Super Cup zinafanyika leo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru zikikutanisha timu za Tanzania na wenyeji, Kenya.

Simba SC watamenyana na Kakamega Homeboyz wakati Singida United watamenyana na Gor Mahia ya Kenya.

Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Jumapili na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park jijini Liverpool, England.

Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.

Bingwa mtetezi ni Gor Mahia ambayo mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.