Samatta afanyiwa kipimo, anusurika

Samatta afanyiwa kipimo, anusurika

11 September 2019 Wednesday 14:39
Samatta afanyiwa kipimo, anusurika

Na mwandishi wetu

KLABU ya KRC Genk ya Ubelgiji imemfanyia uchunguzi wa kitabibu wa goti, mshambuliaji wa timu hiyo, Mbwana Samatta.

‘‘Jopo la madaktari 10 wa klabu yangu kwa pamoja wamenifanyia kipimo cha goti kupitia kipimo cha MRI ,’’ ameandika Samatta katika ukurasa wake wa Instagram

Hatua hiyo ni kufuatia majereha aliyopata katika goti kwenye mchezo wa awali wa kufunzu mashindano ya kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kati ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi.

Katika mechi hiyo iliyochezwa jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2019, Taifa Stars iliitoa Burundi kwa mikwaju ya penati 3-0 baada ya mechi kumalizika kwa sare 1-1 mechi hiyo ilichezwa kwa dakika 120.

Mbwana ambaye ni nahodha wa Taifa Stars, alipata majeraha hayo kunako dakika ya 106 na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Himid Mao ‘Ninja’.

Katika ukurasa wa wake wa Instagram Samatta kaandika;

‘‘Mazungumzo yangu na daktari baada ya vipimo

Daktari na karatasi ya kipimo mkononi.

daktari- ndugu samatta

Mimi- ndio daktari

Daktari-majibu yako yanaonesha....... anachukua miwani anavaa anaguna mh

Mimi-mapigo ya moyo yanaanza kupanda, tumbo linavurugika,haja kubwa inagonga nguo ya ndani.. Daktari-una bahati sana eneo ambalo lilikuwa karibu kuumia lingekufanya ukae nje sio chini ya miez 6 lakini alijapata jeraha zaidi ya mtikisiko kwaiyo siku chache za mapumziko zitakufanya uendelee kucheza

Mimi-shuuuuuuu (nashusha pumzi) sikumbuki niliibana kwa sekunde ngapi.

Daktari-kwaiyo unaweza kuendelea na matibabu na mazoezi

Mimi-asante. So majibu- maumivu sio mkubwa sana na baada ya siku kadhaa nitakuwa tena viwanjani kupambania kombe

Updated: 11.09.2019 14:47
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.