banner68
banner58

Samatta arejesha makali atungua mbili Ulaya

Hapo jana aliweza kuwaacha hoi Wabelgiji baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu sana

Samatta arejesha makali atungua mbili Ulaya

Hapo jana aliweza kuwaacha hoi Wabelgiji baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu sana

14 May 2018 Monday 12:39
Samatta arejesha makali atungua mbili Ulaya

Na Amini Nyaungo

Mchezaji nyota wa Tanzania Mbwana Samatta amerudi kwa kishindo mara baada ya hapo jana kuifungia timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji mabao mawili katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Sporting Charleroi katika uwanja wa Luminus Arena.

Samatta amecheza kwa dakika zote 90 huku akionesha kiwango cha hali ya juu ambapo magoli yake yalifungwa dakika ya 24 na 61.

Makali yake yameonekana kurejea tangu Alhamisi baada ya kutokea benchi na kufunga goli la kusawazisha kufanya matokeo kwenda kwa goli 1-1.

Hapo jana aliweza kuwaacha hoi Wabelgiji baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu sana.

Magoli mengine mawili yalifungwa na Leandro Trossard dakika ya 34 na Dieumerci N'Dongala dakika ya 77.

Magoli yake ya jana yanamfanya Samatta kufikisha magoli 25 katika mechi 88 za mashindano yote aliyocheza KRC Genk.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
super duma 2018-05-25 15:35:34

hongera samata

Avatar
Hassan Kisondo 2018-05-14 21:31:58

Hongera kwa kuipaisha Tanzania.

Avatar
Mudy 2018-05-14 22:24:00

samatta nouma

Avatar
mshana 2018-05-15 18:16:37

hongera sana Samatta kwa kuitangaza vizuri tanzania

Avatar
safisana 2018-07-10 17:12:03

samatta oye

Avatar
Rashidi Mdk 2018-07-13 19:08:09

Hongera Mbwana Ally Samatta Kuitanganza Nchi Yetu Tz Nakutakia Mafanikio Mema Popote Uendapo Nchn France

Avatar
Felimoo Rich 2018-07-26 11:15:45

Samagoal asante kwa kitangaza vema tanzania! Mungu adhidi kukujalia afya tele! Tz-mbeya

Avatar
VENAS 2018-10-03 04:56:05

Hongera Sana Samata Nazielewa Vizuri Kazi Zako Uwanjani