Samatta atua nchini, tayari kwa Afcon 2019

Waziri Mwakyembe usiku Mei 25, 2019 aliwaongoza Watanzania kumpokea mchezaji huyo aliyewasili majira ya saa 9:00 usiku Uwanja wa Ndege Julius Nyerere

Samatta atua nchini, tayari kwa Afcon 2019

Waziri Mwakyembe usiku Mei 25, 2019 aliwaongoza Watanzania kumpokea mchezaji huyo aliyewasili majira ya saa 9:00 usiku Uwanja wa Ndege Julius Nyerere

26 May 2019 Sunday 09:26
Samatta atua nchini, tayari kwa Afcon 2019

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ametua nchini tayari kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.  Harrison Mwakyembe jana usiku Mei 25, 2019 aliwaongoza Watanzania kumpokea mchezaji  huyo aliyewasili majira ya saa 9:00 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

Stars inajiandaa kucheza  katika mashindano ya Afcon 2019  yatakayochezwa nchini Misri mwezi Juni mwaka huu. Ipo kundi moja na timu ya Senegal, Algeria na Kenya.

Samatta ndiye ataongoza kikosi hicho akiwa nahodha.

Tayari kikosi cha Stars chini ya Kocha  Emmanuel Amonike kinatarajiwa kuanza maandalizi kwa ajili ya fainali hizo ambazo  Tanzania inashiriki kwa mara ya pili.Mara ya kwanza ilishiriki mwaka 1982.

Updated: 27.05.2019 14:47
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.