Samatta azungumzia Stars kufungwa Afcon

Samatta azungumzia Stars kufungwa Afcon

24 June 2019 Monday 06:56
Samatta azungumzia Stars kufungwa Afcon


Cairo, Misri
NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema kutojiamini, kutotulia na kushindwa kumiliki mpira kwa muda mrefu ndio sababu ya kufungwa na Senegal

Senegal, ama Simba wa Teranga walishinda  goli 2-0 dhidi ya Stars katika mchezo wa kufungua dimba wa kundi C.

Simba hao waliuanza mchezo kwa kasi, huku washambuliaji wao wakilisakama lango la Stars, na ndani ya dakika 10 za mwanzo wakawa wameshapoteza nafasi za wazi karibia tatu.

"Kweli wachezaji wa Senegal wengi ni 'profeshino' wanacheza ligi kubwa wanajua wanachofanya uwanjani lakini sababu kubwa ya kufungwa kwa Stars ni kutojiamini na kutomiliki mpira kwa muda mrefu, tulikuwa tukipoteza mipira sana, hatukutulia,'' amesema Samatta.

Nayo Algeria ilifanikiwa kuifunga Kenya kwa goli 2-0 na huku winga wa klabu ya Manchester City Riyad Mahrez akifunga goli moja dakika ya 43

Goli la kwanza lilifungwa kwa penati kunako dakika ya 34 na mchezaji Baghdad Bounedjah   Algeria inajiunga na Senegal ikiwa na pointi tatu.

Algeria itajaribu kushinda michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu 1990, walihitaji kushinda mechi hiyo dhidi ya Kenya ambayo ilikuwa inarudi katika michuano hiyo tangu ishiriki mara ya kwanza 2004.

Juni 27, 2019 Algeria itakabiliana na Senegal huku kenya ikichuana na Tanzania baadaye siku hiyo.

Kipa wa Taifa Stars, Aishi Manula aliokoa michomo kadhaa ambayo ingeweza kuleta madhara kwenye lango la Tanzania.

Iliwachukua dakika 28 kwa Senegal kutangulia kwa kupata goli la kuongoza kwa shuti la karibu la mshambuliaji Keita Balde.

Balde ambaye anachezea miamba ya soka nchini Italia, klabu ya Inter Milan aliendelea kuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Stars kwa kosa kosa zake.

Baada ya hali kuzidi kuwa ngumu, kocha wa Tanzania Mnigeria Emmanuel Amunike alilazimika kumtoa Feisal Salum katika dakika ya 43 na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa.
Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika, Senegal ilikuwa imemiliki mchezo kwa asilimia 61, na kupiga mashuti 13 langoni mwa Tanzania.

Tanzania ilikuwa imemiliki mchezo kwa asilimia 39, na kuambulia mashuti mawili kwenye lango la Senegal.

Kipindi cha pili kikaanza kama ilivyokuwa kwa kipindi cha kwanza kwa Senegal kushambulia kwa nguvu langoni mwa Tanzania.

Krepin Diatta aliachia shuti kali katika dakika ya 65  na kumshinda kipa Manula.

Umiliki wa mpira baada ya dakika 90 ulisalia kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza, Senegal 61% na Tanzania 39%.

Hata hivyo kwenye mashuti langoni, Senegal wamepiga michomo 23, kati ka hiyo 13 ikilenga lango.

Tanzania imepiga mashuti 3 na yote hayakulenga goli.

Ni dhahiri kuwa Senegal ambayo ilimkosa mshambuliaji wake tegemezi na nahodha Sadio Mane ingeweza kushinda kwa magoli mengi zaidi.
Baadhi ya mashabiki wa kandanda wameoneka na kuelekeza lawama zao kwa kocha Amunike.

Bado hasira za kuachwa kwa viungo nyota Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu angali zimo kwenye fikra za wengi.

Updated: 25.06.2019 09:19
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
stefano nyati ya masai 2019-07-07 05:49:09

taifa stars walijitahidi zaidi ya mnavyofikili lakini ilishindikana ila mungu mkubwa kukwama leo sio mwisho wa safali tujipe moyo tutafika tu

Avatar
Devi 2019-07-07 10:30:39

Taifa stars kocha hamna lolote