banner68
banner58

Samatta noma, apiga hattrick KRC Genk ikishinda 5-2 dhidi ya Brondby IF ya Denmark

Samatta noma, apiga hattrick KRC Genk ikishinda 5-2 dhidi ya Brondby IF ya Denmark

24 August 2018 Friday 08:47
Samatta noma, apiga hattrick KRC Genk ikishinda 5-2 dhidi ya Brondby IF ya Denmark

NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga mabao matatu timu yake KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Brondby IF ya Denmark katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Europa League.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Samatta amefunga mabao yake katika dakika za 37, 55 na 70 wakati mabao mengine ya Genk yamefungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard kwa penalti dakika ya 45 na ushei na 90 na ushei.

Mabao ya wageni yamefungwa na beki wa Iceland, Hjortur Hermannsson dakika ya 47 na mshambuliaji Mpoland Kamil Wilczek dakika ya 51.

Genk sasa watatakiwa kwenda kuulinda ushindi wao katika mchezo wa marudiano ugenini, Agosti 30 Uwanja wa Brondby.

Timu

KRC Genk: Vukovic, Uronen, Lucumi, Dewaest, Maehle, Berge, Malinovskyi, Pozuelo, Trossard, Samatta na Ndongala/Paintsil dk73.

Brondby IF: Schwäbe, Jung, Hermansson, Kaiser/Tibbling dk78, Mukhtar, Larsson, Wilczek, Christensen/Fisker dk88, Radosevic, Arajuuri na Erceg/Uhre dk70.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Makiya Abubakar 2018-08-24 09:12:18

Hongera Ndugu Yangu Waoneshe Wazungu Kuwa Unaweza Zaidi Ya Hapo, Na Sisi Wa Tz Tuko Nyuma Yako Kwa Dua Njema

Avatar
Leopold Leonard Mtiba 2018-08-26 14:54:11

Hongera Sana Samatta Tukonyumayako Kwa Dua

Avatar
BARAKA 2018-09-14 00:07:23

IDDI