Simba kuipiga bao Yanga kwa Salamba

Ni katika usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara

Simba kuipiga bao Yanga kwa Salamba

Ni katika usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara

23 May 2018 Wednesday 11:29
Simba kuipiga bao Yanga kwa Salamba

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba imeingia miguu miwili kwa mchezaji wa Lipuli, Adam Salamba baada ya Yanga kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo ya Iringa.

Yanga walikuwa wakihitaji huduma ya mshambuliaji huyo ili kuwaongezea nguvu katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini viongozi wa Lipuli ulikataa, ikidaiwa kuwa ni kwa sababu ya uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.

Katika hatua nyingine bado katika kuimarisha kikosi hicho katika kuelekea mashindano makubwa barani Afrika, Simba wanahitaji kumuongeza nyota wa Majimaji Marcel Bonaventure Kaheza ambaye alifunga jumla ya magoli 13 katika Ligi Kuu Tanzania bara iliyomalizika hivi karibuni.

Msemaji wa Simba Haji Manara ameuambia umma wa Watanzania na mashabiki wa timu hiyo kwamba watasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ili kuimarisha kikosi chao.

‘’Tutasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu na tunamuahidi Rais Magufuli tutafanya vile alivyotuelekeza,’’ alisema Haji Manara.

Simba inasemekana itaachana na nyota wake nane ambao wanaonekana hawana msaada kwa timu hiyo.

Moja ya nyota wanaotajwa kukatwa ni pamoja na Haruna Niyonzima, Laudit Mavugo pamoja na Juma Luizio.

Azania Post

Updated: 23.05.2018 11:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.