Simba kula matapishi yake kwa kocha Dylan Kerr

Kerr alifukuzwa Simba mwaka 2016, huenda akarejea iwapo baadhi ya mambo yatatekelezwa

Simba kula matapishi yake kwa kocha Dylan Kerr

Kerr alifukuzwa Simba mwaka 2016, huenda akarejea iwapo baadhi ya mambo yatatekelezwa

12 June 2018 Tuesday 14:11
Simba kula matapishi yake kwa kocha Dylan Kerr

Na Amini Nyaungo

Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba 2015-2016 Dylan Kerr ameonyesha nia ya kutaka kurejea Simba mara baada ya kufanya vizuri na klabu yake ya Gor Mahia ya Kenya katika michuano ya SportsPesa Super Cup.

Kerr ambaye alifukuzwa na Simba mwaka 2016 baada ya mmoja wa kiongozi wa bodi ya timu hiyo kusema kuwa hakuwahi kuona timu mbovu kama ya kipindi cha kocha huyo hivyo hana faida kuendelea kubaki, kauli hiyo imemuumiza hadi kufikia kusema wazi wakati wa fainali ya SportPesa Super Cup.

Kerr amesema kwa kuwa kuna uongozi mpya ndani ya timu hiyo huku mwekezaji mkuu akiwa Mohamedi Dewji hana shaka endapo watamuhitaji kurejea lakini atakuwa na masharti yake endapo wale viongozi waliokuwepo katika bodi ya Simba waondolewe.

Simba bado haijatengua kitendawili cha nani atakuwa kocha mkuu au kama Pierre Lichantree ataendelea kubaki na kazi ya kukinoa kikosi cha mnyama mara baada ya hapo jana kuonekana ukumbini wakati wa tuzo za Mo Simba Awards 2018.

Kerry alizungumza kwa hisia pale aliposema kuwa, “Kuna mjumbe mmoja aliwahi kusema hajawahi kuona Simba mbovu kama yangu, nashukuru kwamba amekuja Kenya na ameona uwezo wa timu yangu ya Gor Mahia.”

“Kama walisema nimekuwa mbovu iweje sasa nina timu nzuri, timu inayofanya vizuri katika mashindano yote,” amesema.

Kwa kauli zake hizi inaonekana baada ya mchezo alifuatwa na baadhi ya viongozi wa Simba kumuulizia kama ataweza kujiunga na timu hiyo ambayo inasaka kocha atakayeendana na kasi ya Simba.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.