Simba kutawala soka la Bongo miaka mitano

Simba kutawala soka la Bongo miaka mitano

19 August 2018 Sunday 11:07
Simba kutawala soka la Bongo miaka mitano

Baada ya timu ya Simba kufanikiwa kuchukua Ngao ya Hisani mbele Mtibwa kwa kuifunga mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, uongozi wa klabu hiyo umetamba kuchukua mataji mengi kwenye ligi.

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ametamba kuwa kuelekea msimu ujao tayari wameshatia baraka baada ya kubeba Ngao hiyo kwa mabao ya Meddie Kagere na Hassan Dilunga.

Manara ameeleza kuwa Simba itatuchukua vikombe vitano mfululizo ili kuzidi kuwaumiza watani zao wa jadi wa jadi Yanga sambamba na kuweka heshima kutokana na upana wa kikosi chao namna ulivyo.

"Huu ni mwanzo mzuri baada ya kuchukua Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Mwanza, kwa sasa mipango yetu ni kuchukua ubingwa mara tano mfululizo ili kujenga heshima ya soka la Tanzania" alisema Manara.

Simba itaanza safari ya kuwania mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara Agosti 22 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Kaimu Rais wake, Salim Abdallah 'Try Again' umesema kikosi walichonacho hivi sasa kitazidi kuwa bora zaidi ya wapinzani wao.

Akizungumza mara baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii kumalizika jijini Mwanza jana, Abdallah alisema kwa namna kikosi ambacho wanacho kitazidi kuonesha matunda kwenye msimu ujao wa ligi.

Kiongozi huyo amefunguka akiamini kitendo cha kuchukua Ngao hiyo mbele ya Mtibwa kimewafungulia njia nzuri ya kuanza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.

"Kwa kikosi hiki tulichonacho kitakuwa bora zaidi na hii ni kutokana na namna uongozi ulivyopambana kusajili wachezaji ambao watakipigania kupata matokeo, ni mwanzo mzuri kuelekea ligi ya msimu ujao" alisema.

Kutokana na kauli ya Kaimu huyo, inaonesha dhahiri shahiri Simba itaonesha upinzani mkubwa zaidi msimu ujao kutokana na upana wa kikosi chake ambapo uongozi umeahidi kufanya makubwa zaidi siku za usoni.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kupitia kwa straika hatari Meddie Kagere na Hassan Dilunga na kuipa timu taji hilo la kwanza ikiwa na Kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Updated: 19.08.2018 14:10
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.