banner68
banner58

Simba nao waibuka sakala la Fei Toto kusaini Yanga na Singida

Simba nao waibuka sakala la Fei Toto kusaini Yanga na Singida

13 July 2018 Friday 12:12
Simba nao waibuka sakala la Fei Toto kusaini Yanga na Singida

Uongozi wa klabu ya Simba umetolea ufafanuzi juu kiungo mchezaji Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' ambaye usajili wake umezua gumzo jana kwa kujiunga na Yanga akitokea JKU kwa kusaini miaka miwili.

Baada ya Toto kuhusishwa kuhitajika na Simba, Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema klabu yao haikuwa na mipango ya kumsajili mchezaji huyo kutokana na kujaza viungo wengi.

Manara ameeleza kuwa Simba ina wachezaji wengi viungo akisema usajili wa mchezaji huyo kwenda Yanga usihusishwe na Simba kwa kuwa hawakuwa na mpango naye.

Toto ametambulishwa Yanga jana ikiwa ni baada ya masaa kadhaa kupitwa kutangazwa na uongozi wa Singida United kuwa wameingia naye mkataba wa miaka mitatu.

Usajili huo ulikuwa gumzo kubwa jana baada ya Yanga kuitisha kikao na wanahabari majira ya saa 10 jioni ili kumtambulisha Toto ambaye alikuwa pamoja na wakala wake na kuleta sintifahamu ikiwa ni baada ya Singida kumtangaza pia.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.