Simba Queens wakabidhiwa bendera ya taifa

Simba Queens wakabidhiwa bendera ya taifa

12 July 2019 Friday 15:04
Simba Queens wakabidhiwa bendera ya taifa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KIKOSI cha Simba Queens kimekabidhiwa bendera ya Taifa tayari kuelekea nchini Ujerumani ambako watafanya ziara ya kisoka ya wiki mbili. 

Hafla ya kukabidhiwa bendera  hio imefanyika leo Julai 12, 2019 katika ofisi za Wizara ya Michezo zilizopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinatarajia kuondoka nchini Jumatatu Julai 15, 2019 na safari hiyo ni maandalizi ya kujiweka sawa baada ya kumaliza ligi ya wanawake ikiwa nafasi ya tatu, hivyo kufanikiwa kupata nafasi ya kwenda kufanya mazoezi ya wiki mbili nchini humo.

Safari ya Simba Queens imedhaminiwa na Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Simba SC.

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Crescentius John Magori amesema pamoja na mazoezi pia watacheza michezo minne ya kirafiki ambapo michezo mitatu itachezwa mjini Hamburg na mwingine mmoja kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Berlin.

Baada ya semina ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wachezaji wetu na michezo ya kirafiki ambayo itasaidia kuandaa kikosi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake, msafara wa Simba Queens utarejea nchini siku ya Alhamisi Agosti mosi, 2019.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.