Simba Queens ziarani Ulaya

Simba Queens ziarani Ulaya

10 July 2019 Wednesday 14:46
Simba Queens ziarani Ulaya

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Timu ya Wanawake (Simba Queens) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumatatu Julai 15, 2019 kwenda nchini Ujerumani kwa ziara ya kisoka ya wiki mbili.

Msafara wa timu hiyo utakuwa na jumla ya watu 16, wachezaji wakiwa 13 na viongozi watatu, ambapo mkuu wa msafara atakuwa ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Asha Baraka.

Wakiwa nchini humo, wachezaji wa Simba Queens watapata nafasi ya kushiriki semina mbalimbali za kijamii ambazo zina lengo la kuwapa mbinu mbadala za kazi ambazo wanaweza kufanya nje ya maisha ya soka.

Pamoja na hilo pia watacheza michezo minne ya kirafiki ambapo michezo mitatu itachezwa mjini Hamburg na mwingine mmoja kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Berlin.

Baada ya semina ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wachezaji wetu na michezo ya kirafiki ambayo itasaidia kuandaa kikosi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake, msafara wa Simba Queens utarejea nchini siku ya Alhamisi Agosti mosi, 2019.

Safari ya Simba Queens imedhaminiwa na Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Simba SC.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.