Simba sasa watangaza kufanya maamuzi magumu

Ni baada ya kuambulia kipigo mikononi mwa Mbao FC

Simba sasa watangaza kufanya maamuzi magumu

Ni baada ya kuambulia kipigo mikononi mwa Mbao FC

21 September 2018 Friday 07:53
Simba sasa watangaza kufanya maamuzi magumu

Baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa CCM Kirumba, jijini Mwanza, uongozi wa klabu ya Simba umewaomba radhi mashabiki wake.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameibuka na kuomba radhi wa wapenzi, mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa namna walivyoyapokea matokeo hayo ya kusitikisha kwao yaliyosababisha kupoteza alama tatu.

Manara amesema kuwa klabu imejipanga kufanya maamuzi sahihi bila ya presha kwani anajua wanasimba wote wameumizwa kufungwa na Mbao ugenini huku akiwataka wawe watulivu kipindi hiki.

"Bodi ya Wakurugenzi, Sekretarieti na Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo (jana).

"Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu, tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi MAKUBWA ya Timu na klabu, nawaomba mtulie katika kipindi hiki" aliandika Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.