Simba wabadili gia angani katika hili

Simba wabadili gia angani katika hili

26 September 2018 Wednesday 07:07
Simba wabadili gia angani katika hili

Uongozi wa klabu ya Simba umesitisha mipango ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kujiwinda na mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Simba itakuwa mwenyeji Jumapili ya Septemba 30 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kusaka alama tatu ikiwa ni harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema kikosi chao hakuna mpango huo na badala yake kitazidi kuendelea na mazoezi jijini humo kwani hawaoni haja ya kwenda Zanzibar.

Manara ameeleza kuwa kikosi kimetoka kanda ya ziwa juzi hivyo hakuna haja ya kuzidi kupoteza tena muda na badala yake kitaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

"Hatuna sababu ya kupoteza muda kwenda Zanzibar, kikosi kitakuwa hapahapa Dar es Salaam na leo kitaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani," alisema.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya awali kuripotiwa kuwa kikosi kingesafiri kuelekea Zanzibar ikiwa ni baada ya watani zao wa jadi Yanga kufunga safari ya kwenda Morogoro.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.