Simba wachukua tena Ngao ya Jamii

Simba wachukua tena Ngao ya Jamii

18 August 2019 Sunday 05:09
Simba wachukua tena Ngao ya Jamii

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

TIMU ya Simba SC imefanikiwa kunyakua tena ubingwa wa kombe la Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam FC kwa goli 4-2.

Mechi hiyo ambayo ni kiashirio cha kuanza kwa ligi kuu Tanzania msimu 2019/20 ilichezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na kuikutanisha Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara na Azam FC mabingwa wa kombe la FA. Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Agosti 23, 2019.

Magoli ya Simba SC yalifungwa na Shibob aliyefunga mawili dakika ya 16 na 22 , Cloutus Chama dakika ya 56 na mwisho likafungwa na Francis Kahata dakika ya 83, huku magoli ya Azam FC yakifungwa na Shaban Iddi Chilunda dakika ya 13 na Frank Domayo dakika ya 78.

Kuchezwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii huwa ni ishara ya kwenda kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2019/2020, wakati ambao Simba SC na Azam FC watakuwa wamemaliza mechi zao za marudiano za kimataifa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.