banner68
banner58

Simba wafunguka wachezaji wao kutimuliwa Taifa Stars

Ismail Aden Rage nae anena

Simba wafunguka wachezaji wao kutimuliwa Taifa Stars

Ismail Aden Rage nae anena

30 August 2018 Thursday 20:26
Simba wafunguka wachezaji wao kutimuliwa Taifa Stars

Uongozi wa klabu ya Simba umesema utafunguka kwa kutoa tamko lake Jumatatu ya wiki kesho juu ya wachezaji wake 6 kuondolewa katika kikosi cha timu ya taifa.

Mabosi wa klabu hiyo wameeleza kuwa kwa sasa hawatakuwa na lolote la kusema ili kuepusha shari na badala yake wanasubiria siku ifike watoe neno lao.

Jana kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao, aliwataja wachezaji 6 wa Simba kuwaondoa isipokuwa Aishi Manula pekee kutokana na kuchelewa kambini.

Kidao alieleza wamemua kufanya hivyo baada ya Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike kukerwa na kuchelewa kwa wachezaji hao kambini.

Wakati huo huo, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amepingana na maamuzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwapiga chini wachezaji 6 Simba katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Rage amesema maamuzi hayo ni ya kuwakosea wachezaji na badala yake akishauri ni vema wangepewa onyo.

Kiongozi huyo wa zamani Simba ameeleza kitendo cha Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike kuwapa adhabu kali wakati wakiwa hawana rekodi ya kufanya hivyo si cha busara na badala yake alitakiwa aende nao taratibu.

Aidha, ameshauri ni vema zaidi kama wangeweza kutwafutwa kupewa onyo na ikiwezekana walau kupigwa hata faini jambo ambalo lingewaamsha na kuwa wanawahi kwa siku za usoni.

"Ni jambo ambalo si sahihi kabisa, nadhani wangeweza kufuatwa na kupewa hata onyo kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuchelewa. Au kama ingewezekana wangepigwa hata faini" alisema.

Updated: 30.08.2018 20:33
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Raphael Robert 2018-08-31 05:56:49

Huyokocha kakurupuka kutoa maamuzi ivi mtu kama erasto,kichuya kapombe lini nidham yao imeshuka waache usimba nauyanga bwana

Avatar
BESAI Y KIMAZI 2018-08-31 18:48:45

huyo koch maamuzi aliochukua sio sahihih.huyo angekua ananyadhifa katika shilikisho la mpirara tz nadhani angeifikisha simba kugum

Avatar
Saidi ibrahim msira 2018-09-02 10:16:46

Kocha amunike yuko sahihi ila kunawachezaji ambao ni wakorofi lakini Nyoni,Kichuya, kapombe yani wachezaji wa simba hawana nidham mbaya kocha angewaonya hata yaye alikuwa mchezaji je yeye hajawahi kuchelewa?inaonekana kuna mtu anampa maneno ya usimc na uyanga.amekubari kuwa kocha afanye anavyo jua asifate mtu atumie akili yake.

Avatar
magembe masunga 2018-09-06 12:56:56

aise kocha alicho kifanya sio sahihi lakin hatunan lakusema labuda wemekuwa wanachelewa kila mara lakin afikilie aache kuangalia timu huo ni usimba na yanga lakini akumbuke hiyo ni timu ya taifa sio yanga wala simba

Avatar
Juma manyanda 2018-09-15 11:34:28

Alichokifaaanya kocha emanuel n sahih manake mchezaj lazma uwe active kw kla xax hap me cwez jua kma n kwel hao wachezaj walikoxa makuxud au n bahat mbaya but cku zjazo tuuweke pendin ucmb na uyanga il 2jenge team ye2 ya taifa coz cc xote ni wamoja!

Avatar
ferdmpanduni@yahoo.com 2018-09-22 12:14:00

Kocha huyu asijisahau siasa za mpira ni ngumu. Mchezaji anamilikiwa na idara nyingi wamiliki hao ndiyo wawajibishwe.

Avatar
Savio nichombe 2018-09-28 20:59:38

Kocha amemezwa na watu fulafulan wasio pemda wachezaj wa smba wanapopata mafanikio