SImba waitaka TFF ijitafakari juu ya suala hili

SImba waitaka TFF ijitafakari juu ya suala hili

02 October 2018 Tuesday 08:47
SImba waitaka TFF ijitafakari juu ya suala hili

Uongozi wa klabu ya Simba umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia upya suala la mapato ya mechi za ligi kwenda kwa mwenyeji pekee.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema suala hilo bado linapaswa kufanyiwa mapitio mapya kulingana na hali ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Manara ameeleza kuwa ni vema TFF ikajaribu kupitia upya kuona faida na hasara zake kwani wanaweza kuja na mawazo mengine ambayo yatakuwa yanalenga kuzipa faida timu zote.

TFF ilitangaza mabadiliko ya mapato yanayotokana na viingilio vya mashabiki uwanjani kwa msimu huu yote kwenda kwa mwenyeji pekee badala ya mgawanyo kwa timu husika.

"Nadhani TFF wanapaswa kuliangalia vema hili suala kwa kulipitia upya ili kuona faida na hasara zake, pengine wanaweza kuja na mtazamo mpya. Ngoja tuone kwa msimu huu pengine wanaweza wakajifunza kitu" alisema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.