Simba wamficha Yondani kusikojulikana

Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema Yondani bado ana mkataba na Yanga hivyo anatakiwa ajue hivyo

Simba wamficha Yondani kusikojulikana

Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema Yondani bado ana mkataba na Yanga hivyo anatakiwa ajue hivyo

30 May 2018 Wednesday 12:33
Simba wamficha Yondani kusikojulikana

Na Amini Nyaungo

Kumekucha baada ya pazia la ligi kuu Tanzania Bara kufungwa na majira ya usajili wa wachezaji wapya kuchukua hatamu.

Habari za usajili zinazidi kupamba moto, bundi anaonekana kusakama klabu bingwa ya zamani wa Ligi kuu bara Yanga, huku habari juu ya wachezaji wake nyota kuzidi kugubikwa na kiza kinene.

Yanga wanaelekea kumpoteza beki wake kisiki wa muda mrefu, Kelvin Yondani ambaye haijulikani alipo, katika kipindi ambacho kikosi cha klabu hiyo ya Jangwani kikiwa katika maandalizi ya kwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya kimataifa yatakayozihusisha klabu za Tanzania na Kenya, hususan zile zinazodhaminiwa na SportsPesa.

Habari za kuaminika zinatanabaisha kwamba, katika harakati za kuendelea kuibomoa Yanga, baada ya Tshishimbi sasa mabingwa wapya wa ligi kuu nchini, Simba wanaelekeza nguvu zao katika kusaka saini ya Kevin Yondani na hivi tunapoandika habari hii, hayupo katika kambi ya klabu yake ya Yanga.

Yondani anaelekea mwisho wa mkataba wake huku na klabu hiyo ya Jangwani, na Simba ikidaiwa kutaka kuidhoofisha Yanga Zaidi kwa kumshawishi akamalizie soka lake huko baada ya unyama walioufanya Yanga 2012 wa kumficha kabla ya kutua Yanga akitokea Simba.

Wachezaji karibuni saba wa kikosi cha Yanga wanakaribia kumaliza mikataba yao, huku viongozi wakijitahidi kuwashawishi kubaki kikosini.

Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema Yondani bado ana mkataba na Yanga hivyo anatakiwa ajue hivyo.

“Kuna tatizo la fedha kweli lakini Yondani bado anamkataba na Yanga hivyo siwezi kuongea zaidi ya hapo,” amesema.

Wachezaji Wengine ambao wapo njia moja ni pamoja na Beno Kakolanya, Said Makapu, Juma Abdul, Nadir Haroub na Andrew Vincent.

Azania Post

Updated: 30.05.2018 13:34
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.